Breaking News

ZARA BEDEL ASIMULIA COVID 19 ILIVYOMTENGANISHA NA DIAMOND PLATNUMZ

 


MWANAMITINDO wa Kimataifa nchini Tanzania aeleze sababu ya kutokuwepo ushiriki wake katika video ya "Baira" ya Diamond platinum.


Zara Bedel amesema anaelewa uwezo wa Diamond platinum katika kazi zake hivyo na kutokana na kuwapa nafasi wanamitindo hasa wakike kwenye video zake nyingi hivyo yeye kama Mwanamitindo alikua ana ndoto ya kufanya nae kazi.

"Nilitakiwa kuwepo kwenye video ya "baila" lakini kutokana na ugonjwa wa uviko 19 ambao ulienea sana nchi ya Italia ambako yalikua Makazi yangu ilinilazimu nirudi nchini hivyo ikapelekea atafutwe Mrembo mwingine na mimi kutoweza kushiriki katika video hiyo."


Hata hivyo Zara amewaambia wanamitindo wanaotamani kufanya kazi zao nje ya nchi kuwa wasiache kujifunza kupitia watu waliofanikiwa na kumtaja Flavian Matata kama mojowapo ya watu ambao alikua akiwatazama.

"Kufika kwangu hapa ni baadhi ya michango kutoka Kwa watu mbalimbali ambao waliweza kufanikisha natimiza ndoto yangu akiwemo Flavian Matata na wengine wengi hivyo ni vyema kujifunza na kusikiliza ushauri wanaokupa watu waliofanikiwa katika tasnia hi."

Pia Zara ameongeza kuwa Kwa Sasa yupo nchini na anatamani kufaya kazi na wasanii watakaopenda kufanya kazi na yeye.

No comments